Kikosi kilichoanza leo hiki dhidi ya Testimony Academy. Matokeo ni Coastal Union 1-0 Testimony Academy. |
Kama kawaida Coastal Union siku zote wanamuweka Mungu mbele. Hapa ni kabla ya kuanza mechi. |
Hawa ndiwo waamuzi wa leo wakiwa na manahodha wa timu zote mbili. |
Sasa imedhihirika wazi vijana wa Coastal Union wamekwenda
jijini Arusha si kushiriki michuano ya soka la vijana Rollingstone Cup, bali
kuchukua ubingwa wa michuano hiyo iliyoanzishwa tangu mwaka 1999 kwa
kushirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 20 na 15.
Ni baada ya kushinda mechi zote tatu za kundi A, bila
kuruhusu bao hata moja kutikisa nyavu zao tangu mechi ya kwanza dhidi ya Young
Life waliyoshinda 3-0, jana walicheza na JKT Oljoro wakawafunga 1-0 na leo
wamehitimisha mzunguko wa kwanza ili kuingia hatua ya robo fainali kwa
kuwachapa Testimony Academy 1-0.
Mfungaji wa bao la leo ni Ally Kipanga mnamo dakika ya 35 ya
mchezo baada ya kupokea krosi murua kutoka kwa mshambuliaji hatari wa Coastal
Union, Ally Nassor ‘Ufudu’ na kutumbukiza gozi hilo la ng’ombe kwa guu lake la
kulia.
Mpaka mapumziko matokeo yaliendele kuwa 1-0 huku vijana wa
Testimony Academy wakionekana kukata tamaa, katika kipindi cha pili kocha
Bakari Shime, ambaye aliamua kuchezesha kikosi
cha pili na kuwapumzisha wachezaji wake hatari ili keshokutwa wacheze hatua ya
robo fainali wakiwa na afya tele katika dakika 55 ya mchezo aliamua kumtoa
kiungo Mohammed Issa ‘Banka’ na kumuingiza mshambuliaji Bakar Mwaita ili
kujihakikishia ushindi mechi ya leo.
Baada ya Shime kuridhika na hali ya mchezo na kuona hakuna
tena dalili ya kupata mabao ilipowadia dakika ya 70 aliamua kumpumzisha Ally
Nassor ‘Ufudu’ na kumuingiza Suleiman Omary.
Mpaka mwamuzi anapuliza kipyenga cha mwisho kuashiria dakika
90 za kawaida zimefikia tamati ubao wa matokeo uliendelea kusomeka 1-0 maana
yake Coastal Union walitimiza point 9 na kuwafanya kushika nafasi ya kwanza katika
kundi A huku wakisubiri kundi B kukamilisha mechi zao leo ambapo mpaka sasa
Simba SC ndiwo wanaoongoza katika kundi B wakifuatiwa na DAREDA kutoka Arusha.
Kundi B ambalo katika kundi hilo Coastal Union watacheza na
mshindi wa pili siku ya Ijumaa Julai 12, lina timu zifuatazo: Simba SC, DAREDA,
Future Star na CIDT.
Kikosi kilichoanza leo ni: 1. Adam mussa. 2. Mtenji Albano. 3. Mohamed Omar. 4. Halfan Mbarouk. 5. Mwaita saleh. 6.Hamis Rashid. 7.Mohamed Isa. 8. Behewa sembwana. 9. Ali kipanga. 10. Ali Nassor. 11. Ayoub semtawa.
Baadaye akatoka Mohammed Issa akaingia Bakari Mwaita, halafu
akatoka Ally Ufudu na kuingia Suleiman Omary.
Mungu ibariki Tanga, Mungu ibariki Coastal Union.
COASTAL UNION
10 Julai, 2013
No comments:
Post a Comment