Thursday, July 18, 2013

Hemed Morocco awapa mazoezi magumu wachezaji wa Coastal Union.

Hapa akizungumza na wachezaji wapya huku 'Batista' na Captain Santo wakisikiliza, hii ni jana uwanja wa Mkwakwani Tanga..
 Hawa wachezaji wapya sijaanza kuwashika majina yao, mliokuwa Tanga mtanisaidia huyu anayetuliza mpira hku 'Batista' akiutamani na 'Boban' kwa mbaali akiwa tayari kumpa msaada 'Batista'.

Anayekimbia na mpira anaitwa Kiemba, ni mchezaji ambaye nilimuona akifanya mazoezi na timu B lakini sasa ataungana na timu kubwa. Selembe kila alivyojaribu kumzuia wapi. Huyu Kiemba ana nguvu, mbio na ana umbo kubwa. Nimesikia anatoka Pongwe.

 Hemed Morocco, wa kwanza kushoto Ally 'Kidi' pamoja kocha mwanafunzi ambaye sikufanikiwa kupata jina lake maana nilimuuliza katibu Kassim Siagi akasema jina lake limemtoka atanipa baada ya mazoezi ila hatukuonana tena. Ni kijana ambaye anasoema ukocha wa mpira na hapo yupo mafunzoni.

Kiingilio ni Sh 500 lakini uwanja unaingia watu wengi sana, huu upande wa jukwaa kuu kote kunajaa. Ama kweli Coastal Union inapendwa.

COASTAL UNION
18 JULAI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA

No comments:

Post a Comment