Uongozi wa Coastal Union unatoa salamu za rambirambi kwa Kiungo
mshambuliaji wa timu hiyo Razak Khalfan kutokana na kifo cha baba yake Mzee
Khalfan kilichotokea jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na blog hii kwa njia ya simu kutoka jijini Tanga
mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Hilal ‘Aurora’ amesema walipata taarifa jana
kuhusiana na msiba wa mzazi wa Razak na wamempa ruhusa kuhudhuria mazishi kwani
tayari alisharipoti kambini.
“Ni kweli Razak amefiwa na baba yake na tayari tumeshampa
ruhusa, uongozi pamoja na wanachama unasikitika sana kuhusiana na taarifa hizo.
Razak Khalfan ni mwenzetu tumekuwa naye kwa amani hivyo msiba wake ni wetu, “
alisema Aurora.
Blog hii imepata taarifa kuwa mzazi wa mchezaji huyo amezikwa
leo alasiri jijini Dar es Salaam katika makaburi ya Mbagala kiburugwa shimo la
mchanga.
Aidha kwa mujibu wa Razak, mzee wake alikuwa akisumbuliwa na
maradhi ya kiharusi ‘stroke’ kwa kipindi kirefu lakini jana alianguka wakati
akiwa msalani na kwa mujibu wa madaktari alivuja damu ndani ya ubongo na
kuganda.
Sote ni waja wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea. Mbele yake
nyuma yetu.
COASTAL UNION
21 JULAI, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
No comments:
Post a Comment