Nahodha wa Coastal Union Jerry Santo
Katika michuano ya kombe la Mapinduzi iliyokamilika tarehe
12 mwezi huu, kulipachikwa mabao 40. ktika mabao hayo kumechaguliwa mabao 5
ambayo yalionekana kungara kuliko yote.
Bao la kwanza ni la mchezaji wa Tusker Fc Khali Aucho, ambae
alilifunga katika mechi dhidi ya Simba Sports Club. Zikiwa zimebaki dakika sita
mpira kuenda mapumziko Aucho aliunganisha krosi ya Edwin Ombasa kwa kiki kali,
nyavu za wekundu wa msimbazi zikatikisika.
Bao la pili kwa ubora ni la mchezaji wa Azam FC Jockins
Atudo, katika mechi ya Azam dhidi ya Miembeni FC. Pia bao hili liliweka rekodi
ya kuwa bao la mapema zaidi katika michuano hiyo ambapo alilifunga katika
dakika ya kwanza ya mchezo kwa nia ya kichwa, Kumbuka Atudo pia ni Mkenya.
Bao la tatu liliingizwa kimiani na mchezaji Ally Mohammed ‘Gaucho’
wa Mtibwa Sugar kwa shuti kali eneo la penalt mpira ukajikunja mithili ya ndizi
ukamuacha Juma Mpongo wa Coastal Union akishindwa kuminyana nayo.
Bao la nne kwa ubora kwenye michuano hiyo inayoadhimisha
shererhe za mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964
liliingizwa kimiani na Kiggi Makasi wa Simba katika mechi yao dhidi ya Bandari kwa mpira wea adhabu
ndogo ambao uliingia wavuni moja kwa moja bila ya kuguswa na mtu yeyote.
Goli hili hata mimi nasadikisha ni la uhakika na linafaa
kuingia katika rekodi ya mabao mazuri, maana siku hiyo ya mechi nilikuwa sipigi
picha nilikaa juu ya jukwaa kuu pembeni yangu alikuwepo kocha mkuu wa Mtibwa
Sugar Mekky Mexime, ambapo tuikuwepo waandishi wengi tunapiga nae stori. Refa alipopiga
filimbi kuashiria ni free kick na mpigaji akawa ni Kiggy Makasi, Mexime akasema
hilo ni goli,
na lisipoingia naondoka nakwenda kulala, sote tukabana pumzi kuona uchawi wa
kocha Mexime, mara mpira huo wavuni huku golikipa akishangaa umempita vipi.
Jerry Santo nahodha wa Coastal Union ndie anakamilisha
orodha hii ya wachezaji watano walioingiza kimiani mabao kwa ufundi katika
mechi ya Coastal dhidi ya Mtibwa Sugar.
Santo ambae pia ni mkenya alipiga shuti la chini likaingia
langoni mwa Mtibwa huku golikipa mahiri wa timu hiyo Hussein Shariff ‘Casillas’
akishangaa.
Kumbuka Coastal union katika michuano hiyo walishinda goli
moja tu katika mechi tatu walizocheza na kufungwa goli moja tu.
Chanzo: Mwananchi tarehe 21 Januari, 2013 jumatatu.
No comments:
Post a Comment