Kocha wa Coastal Union Hemed
Morroco amedhirisha usemi wake kuwa hakuna sababu ya kushindwa game ya leo,
maana anaamini Azam hawana mpira wa kuwafunga baada ya kutoka suluhu ya bila
kufungana na Azam.
Mechi ya pili ya kundi B
iliyokutanisha Coastal kutoka Tanga na Azam kutoka Dar es Salaam katika kombe
la mapinduzi imeisha bila kufungana tofauti na mechi ya awali ya kundi hilo iliyochezwa leo
alasiri kati ya Miembeni na Mtibwa Sugar ambapo Mtibwa walichabangwa mabao 4
kwa ubuyu (4-0).
“mpaka sasa sijui kwanini
wale jamaa walitufunga katika ligi kuu mzunguko wa kwanza, wabovu sana hawana mpira wa
kutisha, huoni hata mgambo waliwafunga mkwakwani. Naamini tumecheza vizuri ila
kuna matatizo kidogo katika safu yangu ya umaliziaji tumekosa magoli ya wazi sana yapo marekebisho
tutayafanya tumeanza vizuri na tutamaliza vizuri watu wa tanga wasubiri
tunakuja na mwari nyumbani,” alisema kocha mkuu wa Coastal Hemed Morroco.
Awali kabla ya mchezo blog
hii ilipewa taarifa na kocha kuwa Solembe amekubaliwa kucheza na ataanza katika
mchezo wa leo..
Coastal leo saa mbili usiku
walishuka dimbani na Azam katika mechi yao
ya kwanza ya kundi B mapinduzi cup. Kikosi cha coastal ni kama
ifuatavyo:
Namba Juma mpongo, mbili Ismail Suma, tatu Othman Tamim, nne
Kibacha Bakari, tano Philip Mugenzi, sita Shengo Ally, saba Suleima Kassim
‘Solembe,’nane Jerry Santo tisa Mohammed Miraji kumi Mohammed Sudi kumi na moja Daniel Lyaga.
Wachezaji wa akiba ni Rajab
Kaumbu, Hamad Hamis, Abdi Banda, Lukindo Gerrard, Razak Khalfan, Maundi petro na Hussein Ibrahim ‘messi’.
Leo Coastal walicheza soka la
kuvutia ingawa walikosa magoli mengi hasa katika dakika ya 41 kipindi cha
kwanza pale Mohammed Miraji alipomimina krosi nzuri ila ikamkuta Selembe
amejisahau huku akiwa yeye na kipa tu mpira ukampita.
Hata hivyo kocha mkuu wa Azam
FC Stuwart Hart alikiri kwamba Selembe ni mchezaji wa kiwango cha juu na
haamini kama mchezo huo uliisha bila kufungana
kwani Coastal walistahili ushindi.
Katika kipindi cha pili
alitoka Selembe akaingia Hussein Ibrahim, pia akatoka akaingia Lukindo Gerald
Unguja, Zanzibar
0713 593894
3/1/2013
No comments:
Post a Comment