Hapa namuona Kassim Suleiman 'Solembe' wa kwanza kushoto, Twaha Ibrahim 'Messi' katikati na Mansour Mansour nyanda la kutumainiwa timu B.... wakisoma gazeti la michezo kuangalia mzunguko wa kombe la mapinduzi.
alalaaaaaaa kumbe kidojembe nae alikuwepo? Hapa akiwa na Mansour na mtoto Messi... alipokwenda kuwaaga bandarini kuelekea Zanzibar.
Timu ya Coastal Union kutoka
Tanga leo imewasili Dar es Salaam katika safari yao
kuelekea Zanzibar tayari kwa michuano ya
Mapinduzi inayoanza usiku wa leo baina ya Simba na Jamhhuri ya Pemba .
Akizungumza na coastalunion
blog kocha mkuu wa Coastal Union Hemed Morroco amesema timu yake ipo vizuri na
tayari kwa michuano kwani timu walizopangiwa nazo zote anazijua aina ya
uchezaji wao.
Coastal ambayo imepangwa
kundi B itacheza na Azam Fc kesho usiku halafu katika mechi nyingine za makundi
itacheza na miembeni na Mtibwa Sukari ya Morogoro.
Hata hivyo midfield ya
kutumainiwa Kassim Suleiman ‘Solembe’ kuna hatihati asicheze katika michuano
hiyo kutokana na suala la kuchukua pesa za mshindi wa tatu michuano ya
Challenge iliyofanyika Kampala Uganda mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza na Coastal Union
Blog Solembe alisema “Mimi sijui chochote lakini nina uhakika nitacheza, maana
timu yangu ya Coastal haijapewa barua yoyote kuhusiana na sakata hilo .
“Kikubwa ninachoweza kusema
ni kuwalaumu viongozi wa mpira wa miguu Zanzibar ZFA kwani hawajui
wanachokifanya maana hata katika timu ya taifa Zanzibar mimi niliitwa tu hata timu yangu ya
Coastal haikushirikishwa. Maana yake hata kama
ningeumia basi timu yangu ndiyo ingewajibika kunitibu,” alisema Solembe.
Akithibitisha kutoshiriki
Solembe kocha Hemed Morroco alisema “Kassim hawezi kucheza hawawezi kumruhusu
wale watu maana bado wana hasira zao. Ila nakuthibitishia wapo vijana ambao
watachukua nafasi yake na watacheza vizuri tu hakuna shaka,.”
Katika hatua nyingine Coastal
imepandisha wachezaji watano kutoka timu B ambao ni golikipa Mansour, Ibrahim Shekue
‘Messi’, Mohammed Miraji ‘Muddy Magoli’, abdi Banda na Nzara.
“Leo wataondoka wachezaji
saba wa timu B lakini ambao wamethibitishwa kupanda moja kwa moja ni watano ila
hawa wawili mwalimu amesema anataka wapate uzoefu, sitokutajia kwa sasa ni siri
ya mwalimu,” alisema mkurugenzi wa ufundi wa timu Nassor Binslum alipozungumza
nab log hii leo.
Makamanda wa coastalunion
blog kesho wataungana na timu ili kuwaletea matukio yote na picha za uhakika.
0713 593894/ 0752 593894
No comments:
Post a Comment