Tuesday, January 1, 2013

Tujikumbushe tulipotoka....

 Mohammed Mwameja 'Tanzania one' kushoto akiwa na Said Kolongo kulia wote matumbo wazi. Mwameja alikuwa golikipa mkali Tanzania hajawahi kutokea, hata hawa kina kaseja wanasubiri... ila sasa Coastal wana mtoto anachipukia anaitwa Mansour huyoooo... waulizeni Simba B..


Mohamed Mwameja,Douglas Muhani,Said salim Kolongo,Ali Maumba,Juma Mgunda,Hemed Morocco,Hussein Mwakuruzo.... Haya wadau wa coastal anzeni kupanga hayo majina nani ndiyo nani. Ila kuna wawili hapo wameachwa maana wachezaji wapo tisa ila majina niliyojaaliwa kuyapata ni saba tu. ila Hussein Mwakuruzo ni huyo alievaa kofia...

Picha zote kwa hisani ya facebook page ya Mbwiga wa mbwiguke msako wa nyani ngedele haponi... midfield kisheti kamaaa anapiga hiviii halaf anafinya... hiyo ndiyo Coastal watu wameshasajiliwa kwa kupewa feni tu au pasi ya mkaa... siku hizi watu wanasajiliwa kwa magari....

Ndugu zaqngu,

Hakika tumeamua kuwapa taarifa kuhusu timu yetu kwa lengo la kuongeza mapenzi na hamasa kwa timu. kama ninavyokariri kila ninapoandika habari zangu, wapo vijana ambao hawaijui vizuri Coastal hivyo hii ni nafasi yao kuanza kupata taarifa za zamani. Tujikumbushe itakuwa ni kama kionjo cha kuwaletea picha ama matukio ya zamani ya Coastal yaliyoikumba timu ama mchezaji.

Mathalan zipo habari kuna baadhi ya wachezaji walisajiliwa baada ya kununuliwa feni chumbani ama pasi ya mkaa ndipo wakakubali kumwagika wino, wamo wachezaji walipasua mipira katika harakati za kufunga ama kuokoa hatari langoni, pia zipo taarifa Juma Mgunda 'kipande cha baba' aliwahi kupasua nyavu alipofunga goli katika uwanja wa mkwakwani dhidi ya watani wao wa jadi African Sports...

kadhalika wapo wanazi wa timu ambao walikubali kufukiwa baharini ili timu ishinde kwa kufuata masharti ya mganga, cha kuchekesha baada ya timu kushinda watu wakamsahau yule mzee kule baharini na maji yakaanza kujaa... vipi ilikuwaje baadae?

Yote hayo tutayathibitisha ukweli wake kwa kukita kambi mjini Tanga na kuzungumza na wazee wa Tanga.....

Tafadhali usiache kumwambia mwenzako juu ya taarifa hizi njema za kuanzishwa blog hii...

DAR ES SALAAM, TANZANIA
costalunion@gmail.com
0713 593894/ 0752 593894
2/1/2013

No comments:

Post a Comment