Monday, January 7, 2013

Kuna kitu niliwaambia nitasema kuhusiana na michuano hii, haya sasa wakati umefika nisikilizeni.



Ndugu zangu,
Najua tumetolewa katika michuano lakini uhalali wa kutolewa kwetu una walakin. Maana mizengwe ilianza siku ya kwanza tu tunawasili hapa Unguja, ni baada ya kugundua hoteli tuliyopangiwa kufikizia ya Laila Nur... iliyo mtaa wa Maisara ndiyo hiyohiyo waliyopangiwa timu ya Mtibwa Sugar ambao tulikuwa nao kundi moja.

Hili ni kosa la makusudi tena limefanywa na mtu anaejua soka, Amani Makungu, ni mwenyekiti wa ZFA, ni mmiliki wa club ya Miembeni ambayo tulikuwa nayo kundi moja, pia alikuwemo katika kamati ya maandalizi ya michuano hii, kama hiyo haitoshi yeye ndie mmiliki wa Hoteli tuliyofikia ya Laila Nur. Kichekesho.

Sasa uwanja tuliopangiwa kucheza mechi ya mwisho wa Mao Tse Dong hauna hadi ya kuchezwa mechi ya kimataifa. Uwanja upo katika hali mbaya na haujafikisha mita mia moja. Hivyo hata FIFA kama wangekuja kuupima basi mchezo wa leo ungekuwa batili, ima ungerudiwa au michuano ingefutwa.

Viongozi wa Coastal wakiongozwa na kocha mkuu Hemed Morroco walijitahidi sana kuomba kbadilishiwa uwanja walau wacheze uwanja wa Amaan saa kumi jioni kwani haukuwa na shughuli yoyote kwa wakati huo lakini waandaaji walipinga bila kutoa sababu za msingi.

Hata hivyo cha kushangaza siku chache zilizopita uwanja huo ulitumika kwa mechi mbili za mchana na jioni iweje leo tu ndiyo iwe tabu kufanywa hivyo?

Sababu; engo lilikuwa ni kuhakikisha Coastal Union wanaaga michuano hiyo kwa namna yoyote ile, maana uwanja huo wa Mao tse Dong wenyewe wanauita Machinjioni. Yaani timu yoyote ya kigeni ikija inawekwa katika uwanja huo ili ifungwe. Marefa nao hawakucheesha kwa kufuata taratibu na kanuni za soka.

Coastal union katika kipindi cha pili walifunga goli baada ya mpira wa kona, lakini mshika kibendera akasema mpira ulitoka nje, lakini nilipozungumza na Dani Lyanga baada ya mchezo kuisha akanambia mpira ule haukutoka.

Haya jamani, yangu ni hayo tu..... tukutane ligi kuu mzunguko wa pili.





                                                  Uwanja hata majukwaa hauna....

                                  Hata vyumba vya kubadilishia nguo hakuna, hii ni mapumziko...

  Amani Makungu mwenyewe ndie huyo muhindi sijui muarabu alievaa saa.. Ni mmiliki wa Miembeni, ni Rais wa ZFA, ni mjumbe wa kamati ya maandalizi Mapinduzi cup na pia leo alikuwa mgeni rasmi katika mechi ya Coastal Union na Miembeni... mhh this is real a facts that will blow your mind.

          Angalia uwanja hata vyoo hauna, wachezaji wa miembeni wakijisaidia haja ndogo kwenye ukuta.


Miembeni wakati wa mapumziko..




COASTAL UNION OFFICIAL BLOG
costalunion@gmail.com
0713593894
8/1/2013
Unguja, Zanzibar

No comments:

Post a Comment