Kocha msaidizi wa Simba SC ya Dar es Salaam
Jamhuri Kihwelu ‘Julio Pereira’ amesema atajiuzulu ikiwa timu yake itafungwa na
Bandari katika mechi yao
ya mwisho katika kundi A kombe la Mapinduzi usiku wa leo uwanja wa Amaan
Unguja.
Kwa mujibu wa Farouk Kareem
ambae ni miongoni mwa waandaaji wa kombe hilo alitangaza jana uwanjani wakati
wa mechi ya Azam na Miembeni iliyoisha kwa Miembeni kubugizwa magoli 3-1 na
Azam, alieleza kuwa Julio amesema atajiuzulu nafasi yake kama kocha msaidizi wa
Simba kwani Bandari si timu ya maana kuweza kuwafunga.
Michuano hiyo inayofanyika
kila mwaka wiki mbili kabla ya tarehe 12 Januari kuadhimisha mapinduzi matakatifu
ya mwaka 1964 Januari 12, lengo ni kusherehekea pamoja kwa kumuondoa Muarabu
katika visiwa vya Unguja na Pemba ambae
aliwatawala kwa karne nyingi.
Timu za Tanzania bara zinazoshiriki michuano hiyo ni Simba SC , Coastal Union,
Azam FC na Mtibwa Sugar, timu moja ya Tusker kutoka nchi jirani ya Kenya ambao ni mabingwa wa soka mwaka jana
nchini humo nayo inashiriki kama mgeni
mualikwa.
Timu za Zanzibar
ni Miembeni, Bandari na Jamhuri ya Pemba . Michuano
ina makundi mawili ambayo ni kundi A yenye timu za Simba
SC , Tusker, Jamhuri ya Pemba
na Bandari, wakati Kundi B zipo timu za Coastal Union, Azam FC, Miembeni na
Mtibwa Sugar.
Mpaka sasa kundi la kifo
limekuwa ni kundi B tofauti na watu walivyofikiria awali kuwa kundi la kifo
lingekuwa ni kundi A ambalo lina timu nzuri tupu hasa baada ya kukusanya
mabingwa watatu Tusker, Simba na Jamhuri ya pemba.
Aidha tofauti na matarajio
katika kundi hilo
timu mbili za Simba na Tusker zina nafasi kubwa ya kuingia hatua ya nusu
fainali kwani timu hizo katika mechi zao mbili walishinda moja na kupata suluhu
moja. Simba walicheza na Jamhuri nakuwafunga magoli 4-2, halafu mechi ya pili
walicheza na Tusker na kutoka suluhu ya
bao moja kwa moja mechi iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu hasa baada ya Simba
kufungwa na Tusker katika mechi ya kirafiki jijini Dar es Salaam wiki moja tu
kabla ya mchezo huo.
Tusker nao katika mchezo wao
wa kwanza waliwafunga Bandari mabao 5, na suluhu moja dhidi ya Simba. Wakati Bandari
wao wamekuwa kama watoto yatima katika kundi hilo kwani wamepoteza michezo yote miwili
dhidi ya Tusker na dhidi ya Jamhuri, wamebaki na mchezo mmoja kibindoni dhidi
ya Simba ambao hata wakishinda magoli 100 hawawezi kupita maana tayari Simba na
Tusker wana point nne wakati wao hawana point hata moja.
Jamhuri kidogo wana matumaini
kwani walipoteza mchezo na Simba na wakashinda mchezo wao dhidi ya Bandari,
hivyo wana point tatu na wakishinda mechi yao
dhidi ya Tusker leo jioni wanaweza
kuendelea na michuano hiyo, lakini tu wanatakiwa waombe ndugu zao Bandari
wawafunge Simba ambacho ni kitu kisichotegemewa. Kwani wakishinda wao watakuwa
na point sita magoli manne, wakati Simba wakishinda watakuwa na point saba. Mmenifaaahaaaamm…?
Sasa tuje kundi B ambalo ni
la kifo, Coastal Union wanatakiwa kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Miembeni
japo kwa goli moja ili wapate point tano, matokeo yoyote mbali ya hayo
yanamaanisha Coastal Union wapo nje ya michuano. Kwani mchezo wao wa kwanza
dhidi ya Azam walitoka suluhu ya bila kufungana, mchezo wa pili dhidi ya Mtibwa
walitoka suluhu ya goli moja kwa moja. Maana yake Coastal Union wana point
mbili na goli moja.
Wakati Mtibwa wao walifungwa
magoli manne na Miembeni katika mchezo wao wa kwanza na kutoa suluhu ya goli
moja na Coastal Union , hivyo wana point moja
na magoli mawili. Wakishinda mechi yao
dhidi ya Azam watakuwa na point nne.
Azama nao wana point nne na
magoli matatu baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Coastal Union halafu
wakashinda mchezo wao dhidi ya Miembeni kwa magoli 3-1. hivyo bado hawana
uhakika wa kupita ingawa wanaongoza kundi, ila tu nao wanatakiwa kwa hali na
mali washinde mechi yao dhidi ya Mtibwa ambapo watakuwa na point saba.
Hata hivyo, Mtibwa
wakiwafunga Azam magoli zaidi ya moja na Azam wakashindwa kufunga goli hata
moja katika mchezo wao maana yake Azam watatoka, kwani Azam wana magoli matatu
tu na point nne, wakifungwa goli 2-0 na
Mtibwa maana yake Mtibwa watakuwa na magoli manne na point nne.
Miembeni wao wana point tatu
na magoli matano, wakifungwa na Coastal Union wametoka, ila wakishinda watakuwa
na point sita maana yake hakuna ubishi wamepita tena kwa kishindo.
Hiyo ni tathmini yangu ndogo
tu kwa namna michuano nilivyoiona, kundi B bado ni gumu halitabiriki. Lakini nimefurahi
sana michuano imeleta
changamoto ingawa yapo baadhi ya mapungufu nitakuja kuandika mapungufu hayo
michuano ikiisha.
COASTAL UNION OFFICIAL BLOG
unguja, Zanzibar
0713 593894
6/1/2013
Kwa timu hii ya mapacha watatu sidhani kama tutashindwa kurudi na kikombe Tanga.
No comments:
Post a Comment