Saturday, January 26, 2013

Tazama habari picha ushindi wa Coastal Union dhidi ya Mgambo JKT ligi kuu bara leo uwanja wa Mkwakwani.

                                         Jerry Santo na Selembe wakiwa wamewekwa mtu kati

                                                        Kikosi cha Mgambo hiki

                                                           Shango kwa jaaam akiminyana.

                                                        Ilikuwa kizaazaa kweli kweli.

 Kona hii ilizaa kona ya pili ambayo ndiyo ilifanya Philip akawainua mashabiki wa Coastal uwanja wa mkwakwani.

                                             Ally Kidi na Morroco wakitoa maelekezo.

                                       Huyu ndie Philip Mugenzi alieifungia Coastal goli la kwanza.

                                                           Kikosi cha Coastal Union hiki.


 Shaaban Kado mpaka mechi inakaribia kuanza kadi yake ilikuwa bado haijaidhinishwa na TFF mpaka mambo yalipowekwa sawa na Meneja Akida Machai.

                                  Tamim akimpongeza Danny baada ya kuweka wavuni bao la pili.

                                                    Benchi la Mgambo likiwa limevurugwa.

 Baada ya kuingia bao la tatu washabiki wa Coastal wakaanza kumwaga radhi. mmhhhhhh....

                                       Tamim akiambiwa na walimu wake umetufaahaaamm?

 Ushindi ilikuwa ni lazima tazama mwalimu Morroco alivyokasirika ingawa timu ilikuwa inaongoza.

                                  Morroco akizungumza na wanahabari baada ya mchezo kuisha.

 Kigoma hiki chini ya Miraji wandi na Nzori... Baadae si Nzori akasusa baada ya vuvuzela lake kuvunjwa? Wandi akataka kupigana na Nzori... mhhh..

                       Kampira kocha wa Mgambo akizungumza na wanahabari kiunyooongeee maskini.




Hapa maalim Unenge na Chuse wakimtuliza Nzori baada ya kukasirika kuona vuvuzela lake limevunjwa. Akaahidiwa atanunuliwa jipyaaa kutoka South Africa.



Na Mwandishi wetu
Leo katika uwanja wa mkwakwani vijana wa Coastal Union wamewaonea ndugu zao kutoka Handeni Tanga Mgambo JKT kwa kuwapigisha kwata ya mabao 3-1 huku mchezo ukiwa umetawaliwa kwa shangwe na umahiri wa kikosi cha kwanza cha Coastal Union.
Goli la kwanza la Coastal Union liliingizwa kimiani dakika ya 18 na Philip Mugenzi kwa njia ya kichwa baada ya kuunganisha mpira safi wa kona uliopigwa na Selembe.
Baada ya kipindi cha kwanza kuisha kwa Coastal Union Kuongoza goli moja, Mgambo walibadilika na kucheza mpira safi wa kuonana kiasi mashabiki wa Coastal walifungwa midomo kabla ya mshambuliaji hatari wa wagosi wa kaya Danny Lyanga mnamo dakika ya 77 ya mchezo kutumia vema makosa ya golikipa wa Mgambo Tonny Kavishe baada ya mpira kumponyoka na kutua miguuni mwa Danny akamramba chenga golikipa na kuutumbukiza mpira kwa kutumia guu lake la kushoto.
Hali ilizidi kuwa mbaya kwa upande wa Mgambo kwani mashambulizi ya kushtukiza kutoka kwa wagozi wa kaya yaliwazawadia bao la tatu lililofungwa na Mahundi mnamo dakika ya 80 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Danny na kuutumbukiza mpira wavuni bila kutumia nguvu na kuwapa jeuri mashabiki wa Coastal Union kuimba ‘taaatu billaaa taaatuuu biillaaa’ huku wengine wakimwaga radhi uwanjani.
Lakini Peter Mwalianzi wa Mgambo aliharibu furaha ya wagosi wa kaya dakika tatu tu kabla ya mchezo kuisha baada ya kutumia vema makosa ya mabeki wa Coastal waliokuwa wameridhika na magoli matatu ambapo mpira ulimponyoka Othman Tamim na kufanya uvivu kugeuka hivyo ukawababatiza wachezaji wa Coastal waliokuwa ndani ya kumi na nane huku golikipa wa Coastal aliesajiliwa katika dirisha dogo kutoka Mtibwa Sugar alipokwenda kwa mkopo kutoka Yanga Shaaban Kado akiwa ametulia golini akisubiri nusura ya Mungu lakini Mwalianzi alinyoosha mguu wake na kuifuta machozi Mgambo JKT katika dakika ya 88 hivyo matokeo mpaka dakika 90 yakawa ni 3-1.
Kwa matokeo hayo Coastal Union imepata point tatu hivyo imefikisha point 25, na kushika nafasi ya nne katika msimamo ambapo nafasi ya kwanza inashikiliwa na Yanga, ya pili Simba, tatu ni Azam FC na nne ni Coastal Union Mtibwa Suga waliokuwa wakishikilia nafasi ya nne wameshuka nafasi moja chini baada ya jana kufungwa na Polisi morogoro katika uwanja wa manungu Turiani. Huu umekuwa mwanzo bora wa mzunguko wa pili wa ligi kuu bara kwa Wagosi wa kaya.
Kikosi cha Coastal Union ilikuwa ni: Shaaban Kado, Ismail Suma, Othman Tamim, Philipo Mugenzi, Mbwana Hamis, Hamis Shango, Joseph Mahundi, Mohammed Mtindi, Jerry Santo, Suleiman Selembe, Danny Lyanga. Baadae walitoka Selembe, Danny, Muddy Magoli kaingia Atupele, Twaha Messi  na Sudi. Na dakika ya 70 mchezaji Mohammed Sudi alipewa kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa Mgambo.
Kikosi cha Mgambo JKT ilikuwa ni: Tonny Kavishe, Salum Mlima, Yassin Awadh, Salum Kipanga, Bakari Mtama, Novat Lufunga, Chande Magoja, Peter Mwalyanzi, Issa Kanduru, Fully Maganga, Nassor Gumbo.
Coastal Union
Tanga, Tanzania
0713 593894

No comments:

Post a Comment