Huyu ndie manyota mwenyewe Rais wa Coastal Hemed Hilal 'Aurora'
Hii ilikuwa fainali ya Coastal B uwanja wa Karume Coastal Vs Azam Fc kwa jaaam namuona mwenyekiti Aurora na mchezaji wa zamani wa Coastal Yanga Bwanga alievaa miwani.
Ndugu zangu,
Sasa dunia inaendeshwa kwa
kutumia mitandao, kuna propaganda nyingi katika kila kitu kuanzia michezo,
siasa na burudani.
Kwa kuzingatia hayo timu ya
Coastal Union ‘wagosi wa kaya’ imeona haja ya kutengeneza blogu ambayo itaweza
kukupa habari zote zinazohusiana na klabu. Kadhalika tutakuwa tunatoa picha za
michezo wanayoshiriki kuanzia ngazi ya taifa na kimataifa lengo likiwa ni
kukuleta karibu na timu yako.
Kwa msaada mdogo ambao blogu
hii itakuwa inaupata kutoka kwa wadhamini wanaoitakia mema timu hii, blogu
itakuwa inakwenda ama inaifuata timu kila inapokwenda.
Hasa ikizingatiwa katika
michuano ya mpira wa miguu Tanzania
bara timu inahitaji kusafiri katika baadhi ya mikoa hivyo blogu itahakikisha
inafika kwa lengo la kupata kile kinachojiri.
Aidha blogu hii itakuwa
suluhisho la kiu yako kuhusiana na baadhi ya taarifa zinazohusu wachezaji,
mathalan umri, nafasi wanazocheza, historia fupi ya mchezaji na mambo mengine
yanayowahusu.
Kadhalika blogu itajitahidi
kupata historia ya klabu tangu kuanzishwa, itahakikisha inauliza wazee wa mjini
Tanga ambao ima walisikia ama kuona harakati za timu hii ikianzishwa na ni kina
nani waliamua kufanya kitendo hicho cha kishujaa kuanzisha timu mahiri kama Coastal Union.
Mafanikio ya timu pia
kitakuwa kitu muhimu, tutajua kikosi kilichoipeleka timu Dar es Salaam kuchukua
kikombe cha ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988, baadae timu ikaenda Kenya
katika Challenge Cup na kushika nafasi ya pili, yote hayo tutahakikisha
tunaangazia kwa mapana yake.
Lengo la kufanya hivi ni
kuwapa mwanga vijana wapya ambao wana mapenzi na timu lakini hawaijui Coastal
Union ni timu ya aina gani. Wapo watu ambao wanaanza kushabikia mpira wa miguu
miaka ya 2000 lakini wanaposikia jina la Coastal Union wanadhani ni timu mpya.
Lakini ukikutana na watu
wanaojua historia ya soka Tanzania
watakuambia Coastal ni timu ya aina gani.
Hivyo karibuni katika blogu
hii na hakika hutovunjika moyo kwa kuitembelea kila siku maana timu yetu ya Costalunionblogspot
itahakikisha inatoa kitu kipya kila siku kwa lengo la kuelimisha na kushawishi
mashabiki wapya wanaopenda kujiunga na timu hii.
DAR ES SALAAM , TANZANIA
1/1/2013
nice step
ReplyDeleteThanx brother we are going.....
ReplyDeleteKwenye banner pameandikwa GLOB, sijui kama mpo sahihi au mlitaka kumaanisha BLOG. Nice step
ReplyDelete