Mwenyekiti Hemed Aurora nae yumo.
Mpongo, Suma, Tamim, Kibacha, Mugenzi, Mahundi, Santo,
Selembe, Razak, Gabriel Barbosa, sudi.
Hicho ni Kikosi cha Coastal Union ambacho kinaongoza goli
1-0 dhidi ya AFC ya Arusha leo katika uwanja wa Mkwakwani ikiwa ni moja ya
mechi za kujipima nguvu kabla ya kuanza mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania
bara.
Mechi ya ufunguzi watacheza na timu ya nyumbani Mgambo
katika uwanja wa Mkwakwani mwishoni mwa mwezi huu.
Goli la kuongoza dhidi ya AFC limefungwa na Mahundi kwa njia
ya kichwa dakika ya 25 ya mchezo halikupokelewa kwa furaha sana kwani mashabiki
wa Coastal wanaichukulia mechi ya leo kama moja ya mazoezi ya kesho ambapo
watakutana na wapinzani wao wa jadi wa muda mrefu African Sports ya Tanga ambao
hawajakutana nao kwa zaidi ya miaka kumi na tano.
Coastal leo wamemchezesha mchezaji wao kutoka Brazil Gabriel
Barbosa ambae anawapa burudani wapenzi wa Coastal kila anapogusa mpira.
Coastal Union
0713 593894
Tanga, Tanzania
No comments:
Post a Comment