Monday, January 28, 2013

Tazama mechi 12 walizobakisha Coastal Union timu, tarehe, kiwanja na mji watakaocheza.

Nahodha wa Coastal Union Mkenya Jerry Santo akiondoa hatari katika lango la timu yake katika mechi ya ufunguzi mzunguko wa pili dhidi ya Mgambo JKT ya Handeni ambapo Coastal waliibuka na ushindi maarufu wa 3-1 katika mzunguko huu ambapo timu zote za juu Coastal ikiwemo zimeshinda goli tatu. Simba, Azam FC na Yanga wote wameshinda tatu tatu katika mechi zao za ufunguzi.



1.    26/01/2013 Mwakwani (Tanga) Coastal Union Vs Mgambo JKT.
2.    03/02/2013 Mkwakwani (Tanga) Coastal Union Vs Tanzania Prison.
3.    09/02/2013 CCM Kirumba (Mwanza) Toto Africa Vs Coastal Union.
4.    13/02/2013 Kaitaba (Bukoba) Kagera Sugar Vs Coastal Union.
5.    20/02/2013 Mkwakwani (Tanga) Coastal Union Vs JKT Oljoro.
6.    27/02/2013 Mkwakwani (Tanga) Coastal Union Vs Ruvu Shooting.
7.    10/03/2013 Uwanja wa Taifa (Dar es Salaam) Simba Vs Coastal Union.
8.    16/03/2013 Manungu (Morogoro) Mtibwa Sugar Vs Coastal Union.
9.    30/03/2013 Azam Complex (Dar es Salaam) African Lyon Vs Coastal Union.
10.     10/04/2013 Mkwakwani (Tanga) Coastal Union Vs JKT Ruvu.
11.     27/04/2013 Mkwakwani (Tanga) Coastal Union Vs Azam FC.
12.     01/05/2013 Mkwakwani (Tanga) Coastal Union Vs Young African.
13.     18/05/2013 Jamhuri (Morogoro) Polisi morogoro Vs Coastal Union.

NB: Endapo timu za Simba na Azam hazitafanikiwa kuvuka hatua mojawapo ya mashindano ya Champions League  & Confederation Cup Orange 2013 ratiba itafanyiwa marekebisho na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.

Nilizungumza na mwenyekiti wa Coastal Union Hemed hilal 'Aurora' akaweka wazi kuwa katika mechi 12 zilizobaki kikosi chake kitacheza mechi 6 nyumbani.

Na watahakikisha historia ya mzunguko w mwanzo haiharibiwi tena kwa kutofungwa mechi hata moja katika uwanja wa nyumbani. maana yake kama maneno ya Aurora yatakuwa ya kweli basi Coastal Union inajihakikishia kumaliza ligi katika nafasi za juu.

Itakumbukwa mzunguko wa kwanza Coastal Union walicheza mechi 13, lakini katika mechi saba walizocheza nyumbani ni mechi moja tu ndiyo waliyoipoteza ambapo ilikuwa ni mechi ya mwisho dhidi ya Dar Young Africans. 

ambapo Coastal union laiti wangemaliza mechi hiyo kwa ushindi wangekuwa na point 25 na kuweza kuwa katika nafasi tatu za juu. Lakini walimaliza kwa point 22 na kufanikiwa kushika nafasi ya tano chini ya Mtibwa Sugar oliyokuwa nafasi ya nne. 
Coastal Union
Dar es Salaam, Tanzania
28/02/2013

No comments:

Post a Comment