Picha hii niliipiga kwa kutumia simu, huyu ni namba kumi yangu ya michuano hii Mohammed Sudi. Ana nguvu balaa, kumbe ni mmpenzi wa ugali. Kila siku analishwa wali nafsi yake inamuuma mskini. Sasa jana nilipokuwa kambini wachezaji wenzie wanajiandaa kuenda kula wali usiku ili wawahi mechi ya Simba na Bandari uwanja wa Amaan, nikamuona Sudi anashangaashangaa.
Nikamuuliza wewe huendi kula na wenzio, akanambia ahha nitaenda lakini ananijibu hivyo huku anamuangalia muhudumu wa hoteli anavyokata matonge ya ugali, muhudumu mwenyewe ni huyo anaeonekana nusu katika picha anachezea simu. jamaa ni mmbara si mzanzibari.
Nikamuuliza au unataka ugali, akajibu haraka ndio. Jamaa bila hiyana akamkaribisha ugali na hapo nafsi yake bardiiiiiii. ahahaaa usifanye mchezo bwana ugali mtamu.
COASTAL UNION OFFICIAL BLOG
costalunion@gmail.com
7/1/2013
0713 593894
Unguja, Zanzibar
No comments:
Post a Comment