Namba tisa ya kutumainika Coastal Mohammed Miraji akitafuta njia.....
Philip Mugenzi akiokoa hatari kutoka langoni mwa coastal...
Jerry Santo nahodha mstaarabu Coastal akiwanyanyasa wachezaji wa Mtibwa Sugar....
Hataari hataariiii... kamatungekuwa wataalam wa vipimo tungejua shuti hili linakwenda umbali gani kwa saa.
Hapa wazaramo tunaita mpate mpatae...
Dany Lyanga akipiga crosi....
Hii ndiyo rafu aliyochezewa Mohammed Miraji "Muddy magoli" ikafanya mchezaji wa Mtibwa kupewa kadi ya njano ambapo alikuwa na kadi nyingine hivyo kuandika kadi nyrkundu. Mbali ya upungufu huo lakini Coastal walishindwa kuwafunga Mtibwa.
Muddy mwenyewe aliechezewa rafu huyoooo anaelekea langoni, huku wachezaji wengine wa coastal wakibishana nani apige adhabu ndogo hii, Hapa namuona Danny, Mohammed Sudi na Tamim.
Nahodha wa Coastal Jerry Santo kutoka Kenya akizungumza na mkenya mwenzie mchezaji wa Tusker. Baada ya mchezo kuisha Tusker waliingia uwanjani kupasha moto viungo. Leo wana mechi dhidi ya Jamhuri ya Pemba (mabingwa wa soka Zanzibar). wakati wenzao wa kundi A wekundu wa msimbazi Simba wana mechi dhidi ya Bandari.
No comments:
Post a Comment