kutoka kulia upande wa nyuma ni Mohammed Miraji, Hussein Twaha 'Messi', Abdi Banda, Hamad Juma, Ally Nassor 'Ufudu', waliochuchumaa mbele ni Mansour Mansour na Ramadhan shame Batista. Hapa amepungua Nzara Ndaro hayupo pichani.
Na Mwandishi wetu
Uongozi wa timu ya Coastal
Union B imefungua milango kwa vijana wanaotaka kujiunga na timu hiyo ya vijana
chini ya miaka 20 kujitokeza ili kufanyiwa majaribio.
Akitoa taarifa hizo meneja wa
timu ndogo Abdulrahman Mwinjuma ‘Ubinde’ mjini Tanga leo amesema kwakuwa timu
ya Coastal Union B ilionyesha mafanikio makubwa katika michuano ya Uhai
mwishoni mwa mwaka jana kwa kumaliza nafasi ya pili hivyo wachezaji wanane wamepata nafasi katika kikosi cha timu kubwa.
“Mazoezi yanaanza siku ya jumatatu
asubuhi tarehe 14 Januari mwaka huu katika uwanja wa Gymkhana mjini hapa (Tanga),
chini ya kocha wake mkuu Bakari Shime ambae pia alichaguliwa kuwa kocha mkuu
katika michuano ya Uhai.
“Timu ina upungufu wa wachezaji wanane ambao walipandishwa kikosi kikubwa kinachojiandaa na mzunguko wa pili wa
ligi kuu Tanzania bara, kijana yeyote ambae ana umri chini ya miaka 20 akitaka
kufanyiwa majaribio awasiliane na mimi kwa namba (0654851612) ama aje katika
klabu ya timu iliyo barabara ya 11 Tanga,” alisema Ubinde.
Wachezaji wanane ambao
walipanda timu kubwa ambayo wiki iliyopita ilikuwa Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la
Mapinduzi na kutolewa katika hatua ya makundi ingawa haikupoteza mchezo hata
mmoja ni;
Aliekuwa golikipa bora wa
michuano ya Uhai Mansour Mansour, Abdi Banda, Ally Nassor, Hussein Twaha ‘messi’,
Hamad juma, Nzara Ndaro, Mohammed Miraji ‘Muddy Magoli’ na Ramadhan Shame ‘Batista’.
No comments:
Post a Comment