Hizo ni moja ya nyimbo za wapenzi wa Coastal Union na African sports zote za Tanga watani wa jadi wa siku nyingi katika soka na cha kutia burudani zaidi wote wanakaa karibu Coastal Union ipo barabara 11 na African Sports ipo barabara 12 Tanga.
Baada ya kupotea katika ramani ya soka kwa siku nyingi siku ya jumapili tarehe 20, januari mwaka huu katika uwanja wa nyumbani kwa timu zote Mkwakwani. zitashuka dimbani katika mechi ya kirafiki lakini pia inaamua kukumbushia upinzani wa jadi na burudani ya soka iliyokosekana kwa zaidi ya miaka kumi mkoani humo.
Mwenyekiti wa Coastal Union Hemed Hilal 'Aurora' anasema siku hiyo uwanja wa mkwakwani utajaa wazee waliokuwa wakitambiana miaka ya nyuma na itakumbusha burudani ya ngoma na nyimbo za watani hao wa jadi zilizokuwa zitia hamasa sana.
kwa upande wake katibu mkuu wa timu ya African Sports anasema timu yake mbali ya kuwa haipo katika ligi kuu ya Tanzania bara kwa miaka mingi lakini hawatakubali uteja wa kufungwa na watani wao wa jadi kwani katika mechi hiyo wanaocheza si wachezaji bali ni timu kwani mechi hiyo ni ya kihistoria.
"Itakuwa ni mechi ya kihistoria kutokana na timu hizi mbili kuwa na wapenzi wengi wa soka mkoani hapa na pia mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na sisi kutokubali kufungwa hali tunajua Coastal Union watacheza kwa tahadhari kulinda hadhi yao ya kushiriki ligi kuu na kuwa na wachezaji wengi wa kiwangu cha juu," alisema katibu wa African Sports Khatib Enzi.
"Hii mechi sisi tunaichukulia kama mechi ya kujipima nguvu tu na matokeo yoyote yatakayotokea tutakubaliana nayo kwani lengo letu hasa ni kukipa makali kikosi chetukinachoshiriki ligi ya TFF ngazi ya mkoa," aliongeza Enzi.
Mechi hiyo itapigwa saa kumi alasiri katika uwanja wa Mkwakwani Tanga mbele ya maelfu ya mashabiki ambao wengi waategemewa kuwa wa umri mkubwa kwani timu mbili hizo mahasimu hawajakutana kwa zaidi ya miaka kumi sasa katika mechi ya ushindani kama hiyo.
blog yako inakuahidi picha za kutosha kwani itakwenda kukita kambi kuanzia siku ya jumamosi ambapo kutakuwa na mechi ya kujipima nguvu kati ya timu ya AFC ya Arusha itakayopigwa saa kumi alasiri katika uwanja huohuo wa Mkwakwani.
Coastal Union
costalunion@gmail.com
Kikosi cha Coastal Union
Dar es Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment