Sunday, January 6, 2013

Wadau wa Coastal tuiombeeni timu yetu leo inacheza mechi ngumu sana....

          Vijana wa coastal wakiwa darasani wanamsikiliza mwalimu Hemed Morroco 'hayupo pichani'

Coastal Union ya Tanga mpaka sasa haijapoteza mchezo hata mmoja katika miwili waliyocheza kwenye michuano ya Mapinduzi mjini Unguja. Hata hivyo hawajashinda mchezo hata mmoja katika miwili hiyo, maana ya maneno haya ni kuwa Coastal ina point mbili tu na hivyo ipo katika hatari ya kupanda boti kesho kurudi bara ikiwa watafungwa ama kutoa suluhu mechi ngumu ya leo dhidi ya Miembeni.

Hata hivyo hatuna budi kuipongeza Coastal kwa hatua waliyofikia maana michuano ilikuwa na mazengwe mengi sitayasema sasa, nitayasema baada ya mechi ya leo kuisha.

Katika kundi B ambalo ni kundi la kifo hakuna hata mmoja mwenye uhakika wa kuingia ama kutoka katika michuano hiyo kati ya timu nne za Azam, Coastal, Miembeni na Mtibwa.

Msimamo wa kundi hilo unaonyesha Azam wanaongoza kundi wakiwa na point nne magoli matatu, inafuata Miembeni ikiwa na magoli matano na point nne, Coastal ina goli moja na point mbili na Mtibwa ndiwo wanaoshika mkia wakiwa na magoli mawili point moja.

Mchezo wa leo utachezwa saa kumi na nusu alasiri kwa saa za Afrika mashariki katika uwanja ninaopenda kuiiita mbovu wa Mao Tse Dong. hakika uwanja ule hauna hadhi kuchezesha mechi ya kimataifa kama hii.

Na haya ni miongoni mwa mazengwe machache nitakayoyaibua baada ya mechi ya leo kuisha....

COASTAL UNION OFFICIAL BLOG
costalunion@gmail.com
0713 593894
7/1/2013
Unguja, Zanzibar

 

No comments:

Post a Comment