Kikosi cha Simba kilichocheza jana usiku dhidi ya Bandari
Unaweza kuita ni dharau, kujiamini kupita kiasi ama dharura. Maana kwa timu kuamua kuondoa wachezaji wake hatari katika michuano ambayo imefikia hatua ngumu ya nusu fainali si jambo la kawaida.
Jana baada ya kutoa suluhu ya 1-1 na Bandari, weundu wa msimbazi Simba walipata jumla ya point tano baada ya kupata suluhu mbili na kushinda mechi moja dhidi ya Jamhuri. Kwa sasa wameungana na Tusker katika kundi A ambayo ina point saba.
Uamuzi wa kuondoa kikosi cha kwanza katika michuano hiyo imefanywa na kocha mkuu wa Simba Mfaransa Patrick Liewing ambapo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alieleza kuwa anawapeleka wachezaji wake Oman kwa ajili ya kambi kujiandaa na mzunguko wa pili wa kigi kuu bara itakayoanza mwishoni mwa mwezi huu.
Liewing alisema anataka kuona kikosi kamili kunakwenda Oman ili kuweza kuwatambua wachezaji wake na kutazama uwezo wao kwani yeye bado ni mgeni katika timu na hajafanikiwa kuwashuhudia wakicheza kikosi kamili kwani ingawa ameweza kuona mechi kadhaa za michuano ya Mapinduzi lakini asilimia kubwa ilikuwa ni watoto wa Simba B ambao waliletwa kupata uzoefu.
Hivyo simba hiyoooo inaondoka Tusker kazi kwenu.....
katika hatua nyingine michuano hii itaendelea leo katika viwanja viwili tofauti vya Mao Tse Dong na Amaan, ambapo Mtibwa sugar watachuana na Azam FC usiku saa mbili katika uwanja wa Amaan, na Coastal Union watachuana na Miembeni 'watoto wa Amani Makungu' katika uwanja mbovu wa Mao Tse Dong saa kumi alasiri.
COASTAL UNION OFFICIAL BLOG
costalunion@gmail.com
0713 593894
7/1/2013
No comments:
Post a Comment